THE FINAL LAP — Real Racing 3 Kufungwa Rasmi (Habari Kamili na Zawadi za Bure)

Hapa kuna  THE FINAL LAP — Real Racing 3 Kufungwa Rasmi (Habari Kamili na Zawadi za Bure)
Habari Wadau,
Baada ya safari ya miaka 12 iliyojaa msisimko, kasi, na ushindani, kampuni ya EA Mobile imetangaza maamuzi magumu ya kusitisha huduma za mchezo maarufu wa Real Racing 3. Huu ni mwisho wa enzi kwa moja ya michezo bora ya mbio za magari kuwahi kutokea kwenye simu.
Nini Kinafanyika na Lini?
Hizi hapa ni tarehe muhimu unazopaswa kuzingatia:
 * Desemba 18, 2025: Mchezo ulishaondolewa kwenye Play Store na App Store (Delisting). Pia, manunuzi ya ndani ya game (In-app purchases) yamesitishwa.
 * Machi 19, 2026: Siku ya mwisho! Seva (Servers) zitafungwa rasmi na mchezo hautachezeka tena kabisa baada ya hapo.
Zawadi ya Shukurani kwa Wachezaji:
Kama sehemu ya kutoa mkono wa kwaheri, update ya mwisho itawapa wachezaji wote zawadi zifuatazo bure:
 * 1,000 Gold.
 * Gari la Audi S1 e-tron quattro.
 * Gari la 2023 Rimac Nevera.
Muhimu: Kama tayari unamiliki magari haya, utapewa Gold ya ziada badala yake. Hakikisha unatumia Gold na R$ zako zote kabla ya Machi 19, 2026.
Jinsi ya Kupata Game Hilo (Download Link):
Ingawa limeondolewa (delisted) kwa wachezaji wapya, wale ambao walishawahi kulidownload huko nyuma bado wanaweza kulirudisha kupitia "Account History" zao. Kwa wale wanaotaka kulidownload kwa mara ya mwisho, tumia link hii:


Jiunge na Channel yetu kwa Mods zaidi:
Tukifika followers 100, nawawekea Mods za Map bure kabisa!

Jinsi ya Kupokea Zawadi Zako (1000 Gold & Cars):
Ili kupata magari ya Audi S1 e-tron quattro, 2023 Rimac Nevera, na zile 1000 Gold, fuata hatua hizi:
Update Game Lako: Hakikisha unatumia version ya mwisho ya Real Racing 3 iliyotoka mwezi huu wa Desemba.
Ingia Kwenye Game (Login): Fungua game na uhakikishe simu yako ina internet ili liweze kuwasiliana na server.
Angalia Notification/Inbox: Ukishaingia tu, utatumiwa ujumbe wa "Token of Appreciation". Ukikubali (Claim), magari na Gold vitaongezwa moja kwa moja kwenye akaunti yako.
Kama Tayari Unamiliki Magari: Usijali! Badala ya gari, utapewa kiasi cha ziada cha Gold kama fidia.
Angalizo: Hakikisha unafanya hivi SASA HIVI kwa sababu baada ya tarehe 19 Machi 2026, servers zitazimwa na hutoweza tena kupata zawadi hizi wala kuingia kwenye game.

1 Comments

Previous Post Next Post