Bus Simulator Tanzania: Game Mpya ya Kibongo Yaanza Kunukia 🇹🇿🎮

 Bus Simulator Tanzania: Game Mpya ya Kibongo Yaanza Kunukia 🇹🇿🎮

Habari za gaming Bongo!

Wakati wengi wetu tumezoea michezo kama Euro Truck Simulator au Bus Simulator Indonesia, sasa kuna dalili za mapinduzi mapya ya gaming kutoka Tanzania.


Hivi karibuni, blmsoftwaretz , developer wa Kitanzania, ameonesha video ya kwanza ya maendeleo (Devlog Test) ya mchezo unaoitwa Bus Simulator Tanzania — mchezo wa simu unaolenga kuakisi mazingira halisi ya usafiri wa Tanzania.

YouTube video 👇

🔍 Nini Kimeonekana Kwenye Majaribio?

Kwa mujibu wa developer, toleo la majaribio linaonesha:

🛣️ Ruti halisi ya Mbezi – Kibaha Bus  (Dar es Salaam)

🚍 Physics za basi (mwendo, kona, breki)

🚗 NPC traffic na magari yaliyopaki

🚀 Kwa Nini Hii Ni Habari Kubwa?

Kwa miaka mingi, gamers wa Tanzania wamekuwa wakitegemea mods kuweka mabasi ya nyumbani kwenye michezo ya nje.

Lakini Bus Simulator Tanzania inalenga kuwa mchezo kamili wa kwanza wa simu unaojengwa kwa mazingira halisi ya Tanzania — hatua kubwa kwa sekta ya game development ya ndani.

Dounload now 

💬 Wewe Unaonaje?

Ni basi gani ungependa kuona likiwepo ndani ya mchezo huu? Katarina, New Force, Tahmeed au jingine?

📢 Endelea kufuatilia Daudi Gaming kwa updates zaidi kuhusu maendeleo ya mchezo huu unaoibukia.

1 Comments

Previous Post Next Post